
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, utafiti kutoka taasisi ya utafiti ya Ebuteli, imebaini kuwa hakuna ugawaji sawa wa majukumu serikalini, tangu kutangazwa kwa baraza jipya la Mawaziri miezi mitatu iliyopita na hivyo kuathiri ufanisi, na utendakazi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii, kwa mujibu wa taasisi hiyo ya utafiti, inaathiri pakubwa utendakazi serikalini na kuwaacha Mawaziri wengi, bila ufahamu wa nini cha kufanya.
Aidha, utafiti huo umebaini kuwa, tangu mwaka 2019, Mawaziri ambao wamekuwa wakihudumu katika serikali zilizopita, bila hata kufahamu majukumu yao na kusababisha, mvutano na hata kuingiliana kwa majukumu, jambo ambalo limesababisha uongozi dhaifu.
Mfano taasisi ya Ebuteli, inaangazia mvutano uliowahi kushuhudiwa kati ya Mawaziri wa mambo ya ndani na yule anayehusika na ugawaji wa rasilimali za serikali mwaka 2023, ambapo walitofautiana kuhusu uteuzi wa wakuu wa idara mbalimbali.
Ili kutatua changamoto hii, Ebuteli inapendekeza mageuzi muhimu serikalini, yatakayosaidia kujenga uwazi lakini pia kupunguza idadi ya Mawaziri ili kuepusha jukumu moja kufanywa na Mawaziri zaidi ya wawili.