
Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa umma, leo Jumatatu, Novemba 10, imeomba kuachiliwa kwa rais wa zamani wa Ufarasa Nicolas Sarkozy chini ya usimamizi wa mahakama wakati wa uchunguzi wa ombi lake mbele ya Mahakama ya Rufaa ya Paris.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Hatari za kushirikiana na kutishiwa kwa mashahidi zinahalalisha ombi la kuwekwa chini ya usimamizi wa mahakama,” ametangaza Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Jamhuri Damien Brunet, akiomba “ombi la Nicolas Sarkozy” la kuachiliwa likubaliwe.
Nicolas Sarkozy, mwenye umri wa miaka 70, amekuwa anafungwa gerezani baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela pamoja na hati ya kukamatwa ikitekelezwa kwa muda kwa kula njama katika kesi ya Libya, kizuizi kisicho cha kawaida kwa rais wa zamani katika historia ya Jamhuri ya Ufaransa, ambacho kilizua mjadala mkali.
Mnamo Septemba 25, Mahakama ya Jinai ya Paris ilimkuta na hatia ya kuwaruhusu washirika wake kimakusudi kumkaribia rais wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi ili kuomba ufadhili wa siri kwa ajili ya kampeni yake ya uchaguzi wa urais ambapo aliibuka mshindi mnamo mwaka 2007. Alikata rufaa mara moja.