Takriban watu kumi wameangamia leo Jumatatu, Novemba 10, katika ajli  kwenye barabara ya Kasumbalesa katika mkoa wa Haut-Katanga. Kulingana na mashahidi, magari mawili yaliyokuwa yakisafiri yaligongana.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Picha zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha maiti kadhaa zikiwa zimelala chini, moja ikiwa juu ya nyingine, huku mingine ikiwa imenaswa ndani ya magari yaliyoharibika.

Kulingana na baadhi ya vyanzo, ajali hii imesababishwa na mwendo kasi kupita kiasi pamoja na barabara inayoteleza kutokana na mvua.

Kufikia saa sita mchana leo, hakuna idadi rasmi ya vifo ambayo imekuwa imetolewa, kulingana na Radio OKAPI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *