Kikosi kazi cha kifedha cha kimataifa (FATF) kimeishauri Pakistan kudhibiti makundi yanayodaiwa kutakatisha fedha na kufadhili ugaidi, kikibainisha kuwa hali hiyo ni tishio katika ukuaji wa uchumi wa Taifa hilo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari nchini Ufaransa, Elisa de Anda Madrazo ambaye ni rais wa FATF alisema nchi lazima ziendelee kutekeleza ulinzi imara ili kuzuia mtiririko haramu wa fedha.

Wakati Madrazo akieleza hayo, vyombo mbalimbali vya habari nchini Pakistan vimeripoti taarifa kuhusu kundi la wanamgambo la Jaish e Mohammad kufadhili ugaidi na utatakishaji fedha licha ya juhudi zinazofanywa na serikali kudhibiti hali hiyo.

‘’Benki ya Pakistan (SBP) inatambua miamala mbalimbali inayofanyika pamoja na biashara haramu kama njia kuu za utakatishaji fedha. Sekta hizi hufanya kazi kwa uwazi mdogo na mara nyingi haziwezi kufikiwa na uchunguzi mzuri wa kisheria,’’

‘’Hali hii inachanganya juhudi za udhibiti, kwa sababu waendeshaji wa haya mambo waliokamatwa Karachi na Peshawar kati ya mwaka 2023 na 2025 wanaendelea kufanya kazi kwenye kivuli. Kugawanyika kwa taasisi kunazidisha tatizo hilo. Ofisi ya kitaifa ya Uwajibikaji (NAB), inategemea makubaliano na watu kukiri makosa jambo ambalo ni gumu kwa sasa,’’ alisema Razak Khan, mmoja wa maofisa wa FATF.

Mtandao wa Dawn nchini Pakistan ulieleza jinsi mahakama kuu nchini humo alivyoonya juu ya vitendo hivyo vya utakatishaji fedha na ugaidi kwamba vinavunja usalama na taswila ya nchi hiyo.

Taarifa ya FATF pia iliangazia uhusiano dhaifu kati ya wasimamizi wa fedha na vyombo vya kutunga sheria vinavyodaiwa kutokuwa na mwenendo mzuri katika usimamizi wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *