Wanasiasa nchini Tanzania wapo kwenye mshangao mkubwa baada ya kuuawa kwa mamia ya waandamanaji, wakati wa maandamano ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baadhi yao waliozungumza na Shirika la Habari la Ufaransa AFP, wanasema wana uonga wa kuzungumzia  kwa uwazi kilichofanyika kwa sababu ya hofu.

Afisa mwandamizi wa serikali ya Tanzania ambaye hakutaka jina lake kutajwa, ameiambia AFP kuwa, matukio yaliyotokea yanatisha na kudokeza kuwa, kuna makaburi ya pamoja katika maeneo ya Kondo  na Mabwepande, ambako waliouawa wanazikwa.

Polisi wa Tanzania wakimvuta mtu wakati wa maandamano kwenye eneo la Namanga mpaka na Kenya.
Polisi wa Tanzania wakimvuta mtu wakati wa maandamano kwenye eneo la Namanga mpaka na Kenya. REUTERS – Thomas Mukoya

Hata hivyo, ripoti hizo haziwezi kuthibitishwa rasmi. Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, Volker Turk, amesema kuna ripoti ya maafisa wa usalama kuchukua miili ya watu waliouawa kutoka hospitalini na mitaani na kuipeleka katika eneo lisilojulikana ili kuficha ushahidi.

Picha ya video za Watanzania, vijana, waliouwa zimekuwa zikionekana kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kurejeshwa kwa mtandao wa Intaneti nchini humo.

Upinzani nchini Tanzania, unasema watu zaidi ya 1,000 waliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama, wakati nchi hiyo ilipokuwa kwenye giza la siku tano, bila uwepo wa Intanenti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *