Rais wa Israel Isaac Herzog, amezuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Felix Tshisekedi. Kabla ya kuwasili Kinshasa, kiongozi huyo wa Israeli alizuru Zambia siku ya Jumatatu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili wamekuwa wakihimiza kuimarika kwa ushirikiano kati ya nchi zao haswa katika masuala ya kidiplomasia, kisiasa, usalama, kilimo, miundombinu na sekta ya kidigitali, masuala ambayo Israel inatajwa kuwa na uzoefu. Rais Tshisekedi alikuwa na kauli hii baada ya kukutana na mwenzake wa Israel.

Mumejua kwamba Israeli ina maendeleo ya juu katika sekta kadhaa, kwa hivyo tunayo fursa nyingi za kujadili ushindi wa ushirikiano wa kimkakati sababu tunaithamini Israeli, na tunathamini amani katika Israeli. ”Alisema Raïs Tshisekedi.

Viongozi hao wawili wanalenga kuimarisha uhusiano kati ya mataifa yao.
Viongozi hao wawili wanalenga kuimarisha uhusiano kati ya mataifa yao. © Ikulu ya Kinshasa

Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais wa Israel Isaac Herzog kuzuru ukanda wa Afrika ya kati na DRC kwa ujumla, alitumia ziara hii kuimarisha ushirikiano kati ya Israel na DRC.

Rais Tshisekedi, nakushukuru kwa mapokezi na ukarimu huu. Tuendelee kutumika pamoja katika roho ya urafiki na udugu tunapoangalia changamoto ambazo ziko mbele yetu, tukiwa na matumaini na imani kubwa na urafiki. ” alisema Rais wa Israel.

Hii ni mara kwanza kwa Rais huyo wa Israel kufanya ziara nchini DRC.
Hii ni mara kwanza kwa Rais huyo wa Israel kufanya ziara nchini DRC. © Ikulu ya Kinshasa

Aidha ziara hii ya kikazi inalenga kuimarisha uhusiano kati ya Raïs Isaac Herzog na Tshisekedi, ambao waliwahi kutana mwaka wa 2021 jijini Jerusalem, huko Israel kabla ya kukutana tena mwezi Januari jijini Davos, Switzerland. 

Kuhusu mzozo wa DRC na inchi ya Rwanda, Rais wa Israel alikaribisha juhudi ya Marekani ya kutatua mgogoro kati ya DRC na Rwanda, akisema kuwa ingekuwa bora mataifa kuzingatia mgogoro huu badala ya kubaki kuilenga sana Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *