Wapalestina 150 wamewasili nchini Afrika Kusini, walikokimbilia kupewa hifadhi kufuatia eneo lao kukabiliwa na vita kwa zaidi ya miaka miwili.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hawa ndio Wapalestina wa kwanza, kuwasili katika ardhi ya Afrika, licha ya kusainiwa kwa mkataba wa kumaliza vita kati ya Israel na kundi la Hamas.
Ndege iliyowabeba Wapalestina hao iliwasili siku ya Alhamisi jijini Johannerbug, lakini ikachukua saa 12 kabla ya kuidhinishwa na kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo.
Polisi wamesema ilichukua muda mrefu kuwaruhusu kuingia nchini humo, kwa sababu pasi zao za kusafiria, hazikuwa na muhuri wa kuonesha walikotokea, na hawakuonesha nia ya kuomba ukimbizi.

Haijafahamika ni nani aliyepanga safari ya Wapalestina hao, baada ya wengine 176 kuwasili nchini Afrika Kusini tarehe 28 mwezi Oktoba lakini wakasafiri kwenda kwenye nchi zingine.
Afrika Kusini ambayo inatoa hifadhi pia kwa idadi kubwa ya Wayahudi, imekuwa katika mstari wa mbele kupigania haki za Wapalestina ambapo mwaka 2023 iliwasilisha kesi kwenye Mahakama ya Kimatafa ya Haki, kuishtaki Israel kwa kutekeleza mauaji ya kimbari kwenye ukanda wa Gaza.