Siku hiyo ya kitaifa ya maombolezo, ama Volkstrauertag kwa Kijerumani, imefunguliwa kwa hotuba ya Rais Sergio Mattarella wa Italia kwenye baraza la chini la bunge la Ujerumani, Bundestag.

Mattarella yuko nchini Ujerumani kwa ziara ya siku mbili, baada ya kupokelewa siku ya Jumamosi (Novemba 15) na mwenyeji wake, Rais Frank-Walter Steinmeier.

Kabla ya hafla hiyo, Rais wa Bundestag, Julia Klöckner, alisema kumbukumbu hiyo inapaswa kuwa na maana kubwa zaidi ya kuwakumbuka tu waliotangulia. 

“Wanaowapa heshima zao wahanga wa vita na machafuko, wale wanaojuwa wapi chuki na upofu huipeleka jamii, wanapaswa kutosalia kimya pale amani na demokrasia vinapotishiwa popote pale duniani,” alisema Klöckner.

Rais huyo wa Bundestag aliita siku hii ya maombolezo kama “wito wenye kupaza sauti kubwa kwetu leo hii, wakati masafa ya kihistoria yanapoongezeka kutoka masaibu ya vita viwili vya dunia na uhalisia wa vita – na, bahati mbaya, hali ya kawaida ya vita barani Ulaya.”

Baada ya hotuba ya Mattarella, Steinmeier naye atazungumza na taifa kama ilivyo ada ya rais aliyepo madarakani nchini Ujerumani tangu mwaka 1952.

Siku ya Maombolezo
Rais Frank-Walter Steinmeier (kushoto) akihudhuria Siku ya Maombolezo mwaka 2024.Picha: Christophe Gateau/dpa/picture alliance

Siku hii imetengwa kuwakumbuka wahanga wote wa machafuko na vita ulimwenguni, wakiwemo wale waliouawa kwenye vita viwili vya dunia na watu walioteswa na utawala wa Kinazi wa Ujerumani kutokana na utaifa, kabila au ulemavu wao. 

Kwa mara ya kwanza mwaka huu, hotuba ya  Steinmeier itawaja makhsusi kabisa wale waliouawa kwa sababu ya jinsia zao au wanavyojitambulisha kijinsia na pia maafisa wa polisi waliouawa wakiwa kazini.

Mkuu wa jeshi wa Ujerumani: Vita na machafuko lazima yakomeshwe

 Siku ya Maombolezo Berlin
Siku ya Maombolezo ya Ujerumani ilivyokumbukwa mwaka 2024 mjini Berlin.Picha: Christophe Gateau/dpa/picture alliance

Kwenye hafla ya kuweka shada la mauwa katika Wizara ya Ulinri ya Ujerumani mjini Berlin, mkuu wa jeshi la Ujerumani, Bundeswehr, alisema siku hii ya maombolezo ni ukumbusho kwamba “vita na machafuko lazima yazuiwe kwa njia zote.”

Insepkta Jenerali Carsten Breuer pia alikuwambuka wanajeshi wa Bundeswehr waliopoteza maisha yao wakiwa kazini.

“Siku hii ya maombolezo ipo kutumbusha kwamba kamwe tusisahau kwamba utumishi huu kwa nchi yetu unaweza pia kugharimu maisha yetu,” aliongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *