Visa hizo hazitotolewa kwa raia wa Angola, Namibia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo.

Hayo yanajiri wakati Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Shabana Mahmood, akitarajiwa kutangaza mageuzi makubwa ya kudhibiti uhamiaji haramu.

Suala la uhamiaji limekuwa pana na linaloleta mgawanyiko katika miaka ya hivi karibuni katika taifa hilo la Ulaya, hatua iliyochochea sehemu kubwa ya raia wake kukiunga mkono chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Reform UK.

Matamshi makali ya Mahnood, yanalenga kuzuwia wahamiaji kuingia Uingereza kutoka Ufaransa kupitia njia za baharini.

Matamshi yake pia yanachukuliwa kama njia moja ya kurejesha imani ya wananchi kwa chama tawala cha Labour, ambayo imeshuka kulingana na kura za maoni. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *