Wanawake na watoto duniani kote wanakabiliwa na ongezeko kubwa la hatari la ukatili na unyanyasaji wa kijinsia, hasa wakati wa migogoro ya silaha, majanga ya asili na dharura nyingine za kibinadamu.

Vitendo hivi hutokea katika maeneo mbalimbali, lakini vinaongezeka zaidi katika mazingira ya dharura na makambi ya wakimbizi ambako mifumo ya ulinzi huwa imevurugika, hivyo kuongeza mazingira hatarishi.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ukatili huu hufanyika kupitia vitendo vya kijinsia vinavyojitokeza wakati wa vurugu, migogoro na changamoto mbalimbali za kibinadamu, na kuwaacha waathirika wakihitaji ulinzi, msaada na hatua madhubuti za kuzuia na kuponya.

Wanawake na wasichana wengi katika hatari ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia nchini Sudan, huku wanawake na wasichana waliokimbia makazi yao, wakimbizi na wahamiaji wakiwa hatarini zaidi.

© UNICEF/Mohamed Zakaria

Wanawake na wasichana wengi katika hatari ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia nchini Sudan, huku wanawake na wasichana waliokimbia makazi yao, wakimbizi na wahamiaji wakiwa hatarini zaidi.

Kuzuia, kulinda na kuponya

Duniani kote, vijana na watoto wengi wasio na idadi ni wahanga wa mienendo mibaya ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji. Ukiukaji huu wa haki upo kila mahali na unavuka mataifa na tabaka zote za jamii.

Watoto, hasa wasichana, wako kwenye hatari kubwa ya kudhalilishwa kingono, kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili, iwe mtandaoni au nje ya mtandao,hali inayoongezeka zaidi wakati wa migogoro ya silaha.

Umoja wa Mataifa unasema katika mazingira ya changamoto nyingi duniani leo,athari za janga la coronavirus“>COVID-19, migogoro, mabadiliko ya tabianchi na majanga, kutokuwepo kwa hatua za kutosha kushughulikia chanzo cha tatizo kama umaskini, ubaguzi wa kimfumo na ukosefu wa usawa kunaendelea kuongeza mazingira yanayowaweka watoto kwenye hatari ya unyonyaji, unyanyasaji na ukatili.

Watoto waliopitia uhalifu huu hukabiliana na madhara ya muda mrefu kwa afya yao ya mwili, akili na maendeleo yao ya kingono. Kiwewe hiki kinaweza hata kufikia kiwango cha mateso au matendo mengine ya kikatili yasiyovumilika.

Waathirika wengi hawasemi wala kutafuta haki, ukarabati au msaada kwa sababu ya aibu. Kwa wengi, madhara ya ukatili wa utotoni huathiri afya zao maisha yote.

Katika Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030, heshima na haki ya mtoto ya kuishi bila ukatili imewekwa kuwa kipaumbele kupitia malengo yanayolenga kukomesha unyonyaji, usafirishaji, mateso na aina zote za ukatili dhidi ya watoto, pamoja na kutokomeza mila hatarishi kama ndoa za utotoni, ndoa za lazima na ukeketaji.

Kuwasaidia watoto na vijana waliopitia ukatili wa kijinsia

Ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na vijana ni ukiukaji mkubwa wa haki zao na tatizo la afya ya umma duniani.

Unaathiri vibaya afya ya mwili na akili ya watoto. Watoa huduma za afya wana nafasi ya kipekee ya kuwapa walioathirika huduma ya huruma na usikivu, jambo linaloweza kuwasaidia sana kupona kutokana na kiwewe cha zahma iliyowapata.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *