Marekani. Wimbo wa Mariah Carey uitwao “All I Want for Christmas Is You” unatajwa kuingiza mamilioni ya dola kila mwaka kwa zaidi ya miaka 31 sasa.

Ripoti mpya kutoka Forbes zinaonyesha Carey hupata takriban $2.5 milioni kila mwaka kutokana na hakimiliki (royalties) za wimbo huo. Mapato yanayotokana na usajili wa wimbo (publishing), mikataba ya matangazo, matumizi ya wimbo kwenye filamu, TV, pamoja na kwenye maonyesho anayofanya Carey.

Aidha Forbes inasema kuwa tangu wimbo huu kutolewa mwaka 1994, Carey amepata takriban dola 60 milioni kama mapato ya moja kwa moja kutokana na wimbo huo, ikijumuisha hakimiliki na rekodi.

Forbes pia imeweka wazi kwamba wimbo huu ni msingi muhimu wa kubrand jina la Mariah Carey kwenye Krismasi, ikimsaidia kuendesha maonesho ya msimu huo, kusaini mikataba ya matangazo, na hata bidhaa zinazohusiana na Krismasi, hivyo kuongeza zaidi kipato chake.

Hata hivyo kutokana na mapato makubwa anayoyapata msanii huyo wimbo huo unaweza kumsaidia Carey kuwa na utajiri wa muda mrefu, kwani unaendelea kufanya kazi kwa ajili yake kila mwaka. Huku wimbo huo ukimuwezesha Carey kuweka historia kwa kuwa msanii anayesikilizwa zaidi msimu wa Krismasi, akijulikana kama ‘Malkia wa Krismasi’.

Wimbo wa ‘All I Want for Christmas Is You’ uliachiwa rasmi Octoba 29, 1994 huku mpaka kufikia sasa video yake ikitazamwa zaidi ya mara milioni 778 katika mtandao wa YouTube

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *