
Kremlin imekataa Jumatano, Novemba 19, kutoa maoni kuhusu ripoti zilizochapishwa na chombo cha habari cha Marekani cha Axios kwamba Washington na Moscow zinaandaa mpango wa amani kwa siri ili kukomesha vita nchini Ukraine.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Hatuna jipya ambalo tunaweza kuwafikishia kwa sasa,” amesema msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov wakati wa mkutano uliohudhuriwa na shirika la habari la AFP.
Kulingana na Axios, ambayo inadai kutegemea vyanzo vya Urusi na Marekani, mpango huo unashughulikia dhamana za usalama kwa Ukraine, usalama barani Ulaya, na uhusiano wa Moscow na Washington, bila kutatua masuala ya eneo.
Shambulio la anga la Urusi laua watu tisa magharibi mwa Ukraine
Angalau watu tisa wameuawa na shambulio la anga la Urusi huko Ternopil, magharibi mwa Ukraine, Rais Volodymyr Zelensky amesema siku ya Jumatano Novemba 19. Hili ni moja ya mashambulizi mabaya zaidi katika mji mkuu wa kikanda tangu kuanza kwa mashambulizi ya Urusi mnamo mwezi Februari 2022.
“Huko Ternopil, majengo ya makazi ya ghorofa tisa yameshambiliwa (…). Katika hatua hii, watu kadhaa wamejeruhiwa na, kwa bahati mbaya, watu tisa wamefariki,” amesema kwenye mitandao ya kijamii.
Usiku wa kuamkia leo, zaidi ya ndege zisizo na rubani 470 za Urusi na makombora yalirushwa dhidi ya Ukraine, Zelensky amesema, na mamlaka ya maeneo mengi yalikuwa yakitathmini uharibifu leo Jumatano.
Kiongozi huyo wa Ukraine amesema mashambulizi hayo yameonyesha kwamba “shinikizo dhidi ya Urusi halitoshi” na akarudia wito wake wa vikwazo vinavyofaa dhidi ya Moscow na misaada ya kimataifa.