
Karibu miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa mpango wa mazungumzo ya kitaifa jumuishi yanayolenga kutatua mgogoro wa kisiasa na usalama mashariki mwa DRC, madhehebu ya kidini ya Kongo yaliyo nyuma ya mpango huo bado yanamsubiri rais kuitisha mazungumzo hyo.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakati Kinshasa na waasi wa AFC/M23 wakisaini makubaliano ya mfumo huko Doha mwishoni mwa juma lililopita, wakifungua njia ya itifaki nane za mazungumzo, na kiongozi wa upinzani Martin Fayulu ameongeza wito wake wa mazungumzo ya kitaifa nchini DRC, hali ya mchakato huu ikoje inayoungwa mkono na madhehebu mbalimbali ya kidini nchini humo?
Karibu miezi mitatu baada ya kupitishwa kwa mpango mazugumzo kufuatia vikao vinne mwezi Julai na Agosti, na kisha warsha ya siku tano na—miongoni mwa wengine—wasaidizi wa rais, madhehebu haya bado yanamsubiri rais aitishe mazungumzo hayo. Lakini Rais Félix Tshisekedi anajizuia kuzungumza.
Tangu mwishoni mwa mwezi wa Agosti, ametoa vidokezo vichache tu kuhusu matakwa yake. Mnamo mwezi Oktoba, mkuu wa nchi alikataa wazo la mazungumzo ambayo yangejumuisha wawakilishi wa “mchokozi.” Wale walio karibu naye pia wanadai kwamba Félix Tshisekedi wanabainisha wakati wa kuandaa tukio hilo bado haujafika. Hali hii imesababisha baadhi ya wapinzani wake kumshuku kwa kutaka kujiweka kwenye maamuzi ya kila kitu, kufafanua mfumo wa mazungumzo, washiriki wake, malengo yake … na hata kuchagua wakati yatafanyika.
Mpango uliojaa vikwazo
Tangu kuanzisha mazungumzo haya mnamo mwezi Februari, makanisa ya Katoliki na Kiprotestanti ya Kongo yamelazimika kushinda vikwazo vingi ili kuyafanikisha. Wawakilishi wao hapo awali walisafiri katika nchi mbalimbali ulimwenguni kukutana na maafisa wa Marekani, Ulaya, na Afrika, pamoja na watendaji wa kisiasa na wanachama wa makundi yenye silaha yanayohusika katika mzozo unaogawanya mashariki mwa DRC. Hata hivyo, kutokana na kwamba Baaraza kuu la Maaskofu wa Kongo (CENCO) na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC) vilichukuliwa kuwa karibu na upinzani, Félix Tshisekedi ameendelea kuwa na mashaka makubwa katika hatua hii.
Ili kutoa kuidjhnisha mchakato huo, alitaka kupanuliwa kwa mpango mzima, akiomba madhehebu mengine ya kidini yashirikishwe ili kuujumuisha zaidi. Lakini hata hili halikutosha: baadaye, wajumbe wa baraza lake la mawaziri waliletwa ili kuboresha dhana hiyo na kupendekeza mpango mpya, ambao uliwasilishwa mnamo Agosti 25, 2025.