
Nchini Libya, kusainiwa kwa makubaliano ya kufadhili uzinduzi upya wa mchakato wa kisiasa kati ya ubalozi wa Qatar huko Tripoli na mwakilishi wa mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa kumezua ukosoajimkubwa. Qatar inashutumiwa na sehemu ya raia na mamlaka pinzani mashariki mwa Libya kwa kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mvutao unazidi kuongezeka kati ya Ujumbe wa Usaidizi wa Umoja wa Mataifa nchini Libya (UNSMIL) na sehemu ya raia wa Libya kufuatia kusainiwa kwa makubaliano mnamo Novemba 17 kati ya balozi wa Qatar huko Tripoli na mwakilishi wa mpango wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa kwa kufadhili uzinduzi upya wa mchakato wa kisiasa. Utiaji saini huo ulifanyika mbele ya Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini, Hanna Tetteh, raia wa Ghana, ambaye alikaribisha mpango huo.
Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu kiasi au aina ya shughuli ambazo makubaliano hayo yatafadhili. Hata hivyo, makubaliano haya yamezua utata ndani ya nchi. Kwa mujibu wa sehemu ya raia wa Libya, Qatar imekuwa na jukumu hasi katika nchi yao tangu mwaka 2011. Doha mwanzoni ilihusika pamoja na NATO katika mashambulizi ya anga dhidi ya Libya na baadaye ikafadhili vyama vingi vya Kiislamu, vikiwemo vyenye msimamo mkali zaidi.
Walibya, wakiwa wamechoka na kuingiliwa na wageni katika masuala ya ndani ya nchi yao bila kukoma, wanaona ufadhili huu kwa mashaka. Wanabainisha unaweza tu kushawishi mchakato wa kisiasa unaopaswa kuzinduliwa upya kabla ya mwisho wa mwaka. Kwa hivyo, kwa wanasiasa wengi wa Libya, UNSMIL si “mpatanishi asiyeegemea upande wowote” tena.
Kambi ya Libya mashariki yakosoa
Kambi ya Libya Mashariki, inayoongozwa na Marshal Haftar, mara moja imechukua fursa hiyo kujiondoa kwenye mazungumzo ya kitaifa. Osama Hammad, Waziri Mkuu wa serikali yenye makao yake makuu Benghazi, ametangaza “mwisho wa ushirikiano na UNSMIL.” Ameungwa mkono na Bunge, ambalo limetaka “mapitio kamili ya jukumu la UNSMIL” nchini Libya.
Kwa upande mwingine, Umoja wa Makabila, ambao una ushawishi mkubwa nchini, umekataa makubaliano hayo, ukisema kwamba UNSMIL imekiuka sheria za kutoegemea upande wowote.
Jibu la ujumbe wa Umoja wa Mataifa: lilibainisha kuwa zaidi ya nchi13 na mashirika ya kikanda yanafadhili programu mbalimbali ili kuimarisha ushiriki wa mashirika ya kiraia katika mchakato wa kisiasa.
Hata hivyo, kulingana na UNSMIL, hii haiwapi “haki ya kushawishi majadiliano” au “kushawishi uchaguzi wa washiriki.”