
Nchini Côte d’Ivoire, zaidi ya watafuta hifadhi 69,000 kutoka Burkinafaso na Mali 1,500 wamepewa hadhi ya ukimbizi katika wiki za hivi karibuni. “Ufunuo” huu wa siri umefichuliwa katika dashibodi rahisi ya kiufundi iliyorushwa mtandaoni mnamo Novemba 20. Hati hiyo imesainiwa na UNHCR, Shirika la Umoja wa Mataida linalohudumia Wakimbizi, na Daara, shirika moja nchini Côte d’Ivoire, linalohusika na usaidizi wa wakimbizi. Kimsingi ni mabadiliko ya kiishara.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Abidjan, Benoît Almeras
Côte d’Ivoire sasa inawahifadhi wakimbizi karibu 80,000, ikilinganishwa na 2,500 hapo awali. Utambuzi huu unatokana na amri ya wizara iliyopitishwa Julai 2, ambayo haikuonekana sana kwenye vyombo vya habari. “Unapaswa kurejelea gazeti rasmi,” serikali imeambia RFI. Hati hiyo, ambayo tuliweza tuliweza kuona, ilikuwa ikisambazwa miongoni mwa mashirika ya kibinadamu kwa wiki kadhaa, kulingana na taarifa yetu.
Hati hiyo inawapa hadhi ya ukimbizi waomba hifadhi waliosajiliwa kuanzia mwezi Mei 2021 na kuendelea. Hawa ni watu waliokimbia vurugu kusini mwa Burkina Faso na Mali ili kutafuta hifadhi kaskazini mwa Côte d’Ivoire.
Afisa kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi (UNHCR) amekaribisha hatua hiyo. “Hatimaye Abidjan inatambua hadhi hii kwa raia wa Burkina Faso na Mali. Wataweza kupata hati za utambulisho na pasipoti maalum ili kurahisisha taratibu na harakati zao.” Kimsingi, sheria ya Côte d’ivoire ya mwaka 2023 kuhusu hadhi ya ukimbizi tayari imehakikisha haki sawa kwa waomba hifadhi, kama vile haki ya kufanya kazi nchini Côte d’Ivoire.
Kulingana na amri ya wizara, Daara, shirika la misaada na usaidizi kwa wakimbizi na watu wasio na uraia, itakuwa na jukumu la kutekeleza programu za kibinadamu kwa wakimbizi hawa wapya. Kulingana na mmoja wa maafisa wa Daara, hadhi ya ukimbizi pia hufungua mlango wa kusaidiwa kurudi kwa hiari katika nchi ya asili. Hii ni vigumu kuiona kutokana na hali ya usalama katika Sahel.