Jeshi la Lebanon limemkamata, siku ya Alhamisi, Novemba 20, Nouh Zaiter, kiongozi mkuu wa dawa za kulevya nchini humo na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa biashara haramu ya dawa za kulevya katika Mashariki ya Kati. Akitafutwa kwa miaka mingi, mtu huyo aliyepewa jina la “Escobar wa Lebanon” na vyombo vya habari alikuwa chini ya vikwazo vya Marekani na Ulaya tangu mwaka 2023.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Lebanon lilimkamata mfalme mkuu wa dawa za kulevya nchini humo, Nouh Zaiter, wakati wa operesheni katika Bonde la Bekaa, linalopakana na Syria, chanzo cha kijeshi kimetangaza siku ya Alhamisi, Novemba 20. Katika taarifa, jeshi lilmetangaza kwamba “limemkamata N.Z., mmoja wa wahalifu wanaotafutwa sana, katika shambulio la kuvizia barabarani kuelekea Knaysseh,” kijiji anachotoka katika jimbo la Baalbek.

Akiwa mmoja wa koo maarufu zaidi za Washia nchini Lebanon, Nouh Zaiter alikuwa akitafutwa kwa miaka mingi na alikuwa chini ya hati nyingi za kukamatwa, anaripoti mwandishi wetu huko Beirut, Paul Khalifeh. Alikuwa akifuatiliwa na yombo vya sheria vya Lebanon, ambavyo vilitoa hati kadhaa za kukamatwa dhidi yake na kumhukumu bila kuwepo kwa mashtaka kadhaa ya biashara ya dawa za kulevya. Mnamo mwezi Machi 2024, mahakama ya kijeshi pia ilimhukumu kifo kwa kumpiga risasi askari wa Lebanon, na kumuua mmoja wao.

Akihusishwa na uzalishaji na usafirishaji nje wa Captagon, mfanyabiashara huyo wa dawa za kulevya aliongoza himaya halisi katika eneo alilozaliwa, akitengeneza na kusafirisha dawa za kulevya, ikiwa ni pamoja na Captagon, dawa sawa na amfetamini.

Akishutumiwa kupanua biashara ya Captagon katika Mashariki ya Kati na mataifa ya Ghuba, kwa kushirikiana na maafisa wa utawala wa zamani wa Syria, Nouh Zaiter alishukiwa kuwa na uhusiano na Hezbollah. Chama cha Washia kimekuwa kikikataa uhusiano wowote na Zaiter au ulanguzi wa dawa za kulevya. Lakini mfalme huyo wa dawa za kulevya mara nyingi alionyesha hadharani uungaji mkono wake kwa chama hicho.

Wakati wa vita vya Syria, alirekodiwa akiwatembelea wapiganaji wa Hezbollah katika eneo la Qalamoun nchini Syria na kutangaza kwamba alikuwa akiwaweka watu wake mikononi mwa katibu mkuu wa zamani wa chama hicho, Hassan Nasrallah.

Akiwa mtu mwenye utata mkubwa, mfanyabiashara huyu mwenye umri wa miaka 48 alipenda kujionyesha kama mtu wa Robin Hood. Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Lebanon na vya kigeni, alidai kusambaza sehemu ya utajiri wake aliokusanya kinyume cha sheria kwa wakazi wa kijiji chake na watu wa ukoo wake.

Nouh Zaïter alikamatwa bila walinzi wowote. Alijisalimisha kwa jeshi la Lebanon bila upinzani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *