Nchini Niger, kituo cha polisi kilishambuliwa mnamo Novemba 19 katika mkoa wa Tera, magharibi mwa nchi. Kulingana na vyanzo vya usalama, polisi wapatao ishirini waliuawa, na wengine wapatao thelathini walijeruhiwa. Miongoni mwa waathiriwa ni mkuu wa kikosi hicho.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Magari yaliharibiwa au kuchukuliwa na washambuliaji. Hakuna idadi rasmi ya vifo bado haijatolewa, lakini kulingana na mwanaharakati aliye karibu na serikali, magaidi 56 waliuawa. Shambulio hilo lilitokea zaidi ya mwezi mmoja baada ya Jenerali Tiani kufanya zira katika eneo hilo.

Mazishi yalifanyika mnamo Novemba 20 katika makaburi ya Waislamu huko Niamey, mji mkuu wa Niger, yakihudhuriwa na familia, siku moja baada ya shambulio dhidi ya kituo cha polisi karibu na mji wa Garbougna, katika mkoa wa Tera. Kituo hicho kina maafisa wa polisi kadhaa wa vikosi maalum vya uingiliaji kati wa haraka.

Shambulio hilo lilidaiwa na JNIM, kundi llinalodai kuunga mkonoo Uislamu na Waislamu, ambalo ni mshirika wa Al Qaeda na moja ya makundi mawili yanayoendesha harakati zake katika eneo la mpaka wa tatu, kwenye makutano ya Niger, Burkina Faso, na Mali, pamoja na ISIS, Dola la Kiislamu huko Sahel.

Eneo hili mara nyingi hukumbwa na mashambulizi, kama lile la mwezi Juni lililolenga msikiti katika mji wa Manda, katika mkoa huo, na kusababisha vifo vya watu 70.

Mwezi uliopita, Jenerali Abdourahamane Tiani alizuru Tera. Katika hotuba yake, mkuu wa Kamati ya Kitaifa ya Kulinda Nchi (CNSP) alisisitiza umuhimu wa dhamira ya vikosi vya ulinzi na usalama na akasifu kujitolea kwao katika kuwalinda raia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *