Jumla ya raia 89 waliuawa katika kipindi cha wiki moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakati wa mashambulizi kadhaa ya waasi wa Uganda wa Allied Democratic Forces (ADF), kundi ambalo lilitangaza utii kwa kundi la Islamic State, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) umetangaza mnamo Novemba 21, 2025. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

ADF ilifanya mashambulizi haya “mabaya sana” kati ya Novemba 13 na 19 katika maeneo kadhaa katika wilaya ya Lubero, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, MONUSCO imesema. 

Katika mkutano wa mwisho wa ICGLR huko Kinshasa, wakuu wa nchi walitambua ADF kama tishio la kigaidi la kikanda na kutoa wito wa kuimarisha operesheni za pamoja za DRC-Uganda, pamoja na kupeana taarifa za kijasusi, udhibiti wa mipaka, na kanuni zinazohusiana na usalama wa mtandaoni na teknolojia kama vile ndege zisizo na rubani na sarafu za kidijitali.

Habari zaidi zinakujia…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *