Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ametoa wito siku ya Alhamisi, Novemba 20, kwa “amani yenye heshima,” baada ya mkutano na afisa mkuu wa Marekani aliyemwasilishia mpango wa Washington wa kukomesha mashambulizi ya Urusi. Mpango huo unajumuisha makubaliano muhimu kwa Urusi, hasa yale ya kieneo.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ukraine inahitaji amani. […] Amani yenye heshima, ili hali iheshimu uhuru wetu, uhuru wa eneo letu, na heshima ya raia wa Ukraine,” Zelenskyy amesema katika hotuba yake ya kila siku iliyorushwawa kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kukutana na Waziri wa Jeshi la Marekani Daniel Driscoll. Mpango wa hivi karibuni uliowasilishwa na Washington unaonekana kutimiza matarajio ya Moscow, huku jeshi dogo na lisilo na vifaa vya kutosha la Ukraine likijitahidi kudhibiti kusonga mbele kwa Urusi.

Ofisi ya rais wa Ukraine ilibainisha muda mfupi kabla kwamba Volodymyr Zelenskyy anapanga kujadili “katika siku zijazo” na mwenzake wa Marekani, Donald Trump, “chaguzi za kidiplomasia zinazopatikana na mambo muhimu kwa amani.” “Tuko tayari kufanya kazi kwa njia ya kujenga na upande wa Marekani na washirika wetu barani Ulaya na kote ulimwenguni ili kufikia amani,” Ofisi ya rais wa Ukraine imeongeza.

“Rais (Trump) anaunga mkono mpango huu. Ni mpango mzuri kwa Urusi na Ukraine, na tunaamini unakubalika kwa pande zote mbili,” msemaji wa Ikulu ya White House Karolina Leavitt alisema siku ya Alhamisi.

Rasimu ya mpango yenye pointi 28

Mpango wa amani uliopendekezwa, unaoungwa mkono na Washington na ambao shirika la habari la AFP limeona nakala yake, unasema kwamba Crimea, pamoja na maeneo ya Donetsk na Luhansk mashariki mwa Ukraine, “yatatambuliwa kama maeneo ya Urusi, ikiwa ni pamoja na Marekani.” Kulingana na mpango huu wa pointi 28, maeneo mengine mawili, Kherson na Zaporizhzhia kusini, yangegawanywa katika mstari wa mbele wa sasa.

Nakal hiyo pia inaeleza kwamba jeshi la Ukraine litakuwa na wanajeshi 600,000 pekee, ambapo NATO ingejitolea kutoweka wanajeshi nchini Ukraine, na kwamba ndege za kivita za Ulaya zitakuwa na makao yake nchini Poland. Taarifa hii pia iliripotiwa na chombo cha habari cha Marekani cha Axios. Kulingana na vyombo vya habari vya Marekani, mpango huo pia unaitaka Ukraine kutambua Kirusi kama lugha rasmi ya pili na kurudisha haki za Kanisa la Orthodox, ambalo liko chini ya mamlaka ya  Moscow.

Urusi pia inapinga vikali uwepo wowote wa wanajeshi wa NATO nchini Ukraine, pamoja na kujiunga kwa Kyiv na Muungano huo. Kyiv, kwa upande wake, inadai dhamana ya usalama kutoka Magharibi, ikiwa ni pamoja na wanajeshi wa Ulaya katika ardhi yake, ambayo mpango wa Marekani, kulingana na ripoti za vyombo vya habari, ungeizuia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *