
Kiongozi wa upinzani nchini Cameroon Tchiroma Bakary amekimbilia nchini Gambia baada ya uchaguzi uliopingwa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wizara ya Habari ya Gambia imesema kuwa inamkaribisha kwa muda kiongozi huyo wa upinzani wa Cameroon Issa Tchiroma Bakary baada ya uchaguzi uliokumbwa na mzozo nchini mwake ambao ulishuhudia Rais wa muda mrefu Paul Biya akishinda muhula wa nane, na kusababisha maandamano mabaya.
Aidha taarifa kutoka kw awizara hiyo zinasema kuwa Tchiroma aliwasili katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi mnamo Novemba 7 na atakaa nchini humo kwa misingi ya kibinadamu tu na kwa lengo la kuhakikisha usalama wake.
Gambia inafanya kazi na washirika wa kikanda kama vile Nigeria kuunga mkono matokeo ya amani na mazungumzo baada ya mvutano wa matokeo ya uchaguzi nchini Cameroon.
Hiyo jana,msemaji wa Tchiroma, Alice Nkom, alithibitisha kuwepo kwa kiongozi huyo wa Upinzani nchini Gambia.
Upinzani nchini Cameroon umepinga matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 12 uliompatia ushindi Rais Paul Biya, ambaye ana umri wa miaka 92. Hata hivyo Mpinzani wake Tchiroma alipinga ushindi wake