
Muungano wa nchi zinazosaidia upatikanaji wa chanjo duniani kwa nchi masikini, Gavi, Pamoja na shirika la kuhudumia watoto UNICEF wamefikia makubaliano mapya kuhusu bei, ambapo yatashuhudia kupungua kwa gharama ya chanjo muhimu ya malaria na kuwezesha kuwalinda watoto karibu milioni saba ifikapo mwaka wa 2030, mashirika hayo yalitangaza siku ya Jumapili.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Chini ya makubaliano hayo, bei ya chanjo ya R21/Matrix-M itashuka hadi dola 2.99 kwa kila dozi ndani ya mwaka mmoja – punguzo linalotarajiwa kuokoa dola milioni 90.
Chanjo zote mbili za malaria zilizopendekezwa na WHO, R21/Matrix-M na RTS,S, zimeonesha kupunguza maambukizi kwa zaidi ya nusu katika mwaka wa kwanza, ambapo watoto milioni 50 watakuwa wamechanjwa ifikapo mwisho wa muongo huu
Hadi sasa zaidi ya dozi milioni 40 za chanjo ya malaria tayari zimetolewa kupitia programu zinazoungwa mkono na Gavi, huku nchi 24 za Afrika zikijumuisha chanjo ya malaria katika chanjo ya kawaida.
Ugonjwa wa Malaria unabaki kuwa moja ya magonjwa hatari zaidi duniani, ambapo mwaka 2023, ulisababisha vifo vya watu takribani laki 5 na elfu 97, idadi kubwa ya waliofariki wakiwa ni watoto barani Afrika, unicef ikisema mtoto mmoja hufa kutokana na ugonjwa huu kila baada ya dakika moja.