Chini ya makubaliano hayo, bei ya chanjo ya R21/Matrix-M itapungua hadi  dola 2.99 kwa dozi ndani ya mwaka mmoja  punguzo ambalo linatarajiwa kuokoa hadi  dola milioni 90. Akiba hii itawawezesha nchi kupata zaidi ya dozi milioni 30 za ziada katika miaka mitano ijayo yamesema mashirika hayo.

“Tangazo hili ni mfano thabiti wa kile ambacho Muungano wetu wa Chanjo unakifanya vyema zaidi,” amesema An Vermeersch, Afisa Mkuu wa Programu na Masoko ya Chanjo wa Gavi.
Ameongeza kuwa “Tunatumia ubunifu wa kifedha na ushirikiano ili kupata chanjo nafuu zinazoweza kulinda watoto vyema zaidi dhidi ya moja ya chanzo chavifo vingi Afrika.”

Karibu vifo 600,000 vya malaria mwaka 2023

Mashirika hayo yamesema malaria bado ni moja ya magonjwa ya kuambukiza yenye kuua watu zaidi duniani.

Mwaka 2023, ilisababisha takribani vifo 597,000, wengi wao wakiwa ni watoto wachanga barani Afrika. Kila dakika, mtoto mmoja anakufa kutokana na ugonjwa huu.

“Idadi ya vifo kama hii inahitaji hatua,” amesema Leila Pakkala, Mkurugenzi wa Idara ya ugavi ya UNICEF.
“Katika kipindi cha kupungua kwa msaada wa kimataifa, UNICEF imeamua kushirikiana na wadau kuhakikisha chanjo za kutosha zinapatikana kwa bei nafuu ili kulinda watoto.” Ameongeza

Mtoto mwenye umri wa miezi sita anapata chanjo ya kwanza ya malaria huko Gedaref, Sudan.

© UNICEF/Ahmed Mohamdeen Elfatih

Mtoto mwenye umri wa miezi sita anapata chanjo ya kwanza ya malaria huko Gedaref, Sudan.

Ushirikiano wa fedha na hatua za haraka

Makubaliano haya mapya ya bei yametokana na malipo ya awali kupitia Kituo cha kimataifa cha ufadhili kwa ajili ya chanjo (IFFIm), kinachobadilisha ahadi za muda mrefu za wafadhili kuwa fedha za awali.

Hii inaupa Muungano wa Chanjo Gavi uwezo wa kuchukua hatua haraka pale fursa kubwa za soko zinapoibuka.

“IFFIm ipo ili kubadilisha tamaa kuwa hatua,” amesema Ken Lay, Mwenyekiti wa Bodi ya IFFIm.

“Makubaliano haya yanaonesha jinsi ubunifu wa kifedha unavyoweza kufungua fursa zinazookoa maisha.”

Malengo makubwa ya chanjo

Zaidi ya dozi milioni 40 za chanjo ya malaria tayari zimegawiwa kupitia programu zinazoungwa mkono na Gavi, na nchi 24 za Afrika sasa zinajumuisha chanjo ya malaria katika ratiba ya kawaida ya kinga za watoto.
Mahitaji ni makubwa, nchi 14 ziliingiza chanjo hii kwa mara ya kwanza mwaka jana, na nyingine saba zimefanya hivyo mwaka 2025.

Kupungua kwa bei kunatarajiwa kusaidia Gavi kufikia lengo la kutoa chanjo kamili kwa watoto milioni 50 zaidi dhidi ya malaria kufikia mwisho wa muongo huu.

Chanjo zote mbili za malaria zinazopendekezwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, za R21/Matrix-M na RTS,S, zimeonesha kupunguza kesi za malaria zaidi ya nusu katika mwaka wa kwanza baada ya chanjo, huku kinga zaidi ikifuata baada ya dozi ya nyongeza.

Kwa familia na mifumo ya afya ambayo tayari iko chini ya shinikizo kutokana na ugonjwa huu, upanuzi huu unaweza kuleta mabadiliko makubwa.
“Hii ni kuhusu kumpa kila mtoto nafasi sawa ya kupata kinga,” amesema Lay akiongeza kuwa “Ni kuhusu kuokoa maisha sasa, si miaka ijayo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *