Unaweza kujiuliza ni kwa nini? Bila shaka sababu ni kwamba Geraldine alikata tamaa ya maisha baada ya kukumbwa na ukatili wa kingono. Ukisikia nasema teacher Regina, anamaanisha mwalimu Regina.
“Kama kuna mwanamke yoyote ananisikia ambaye amepitia dhuluma za kijamii asijitenge, asikae mbali na watu, asikae pekee yake. Kama nisingepitia shirika hili la Forum For Women nizungumze na Mwalimu Regina saa hii singeweza kuishi. Sijui ningekuwa wapi.”
Taasisi ya FODDAJ inawasaidia wanawake kupambana na ukatili wa kijinsia
Ukatili wa kijinsia aliokumbana nao ulisababisha aghubikwe na hofu kubwa hata hakutaka kupata mtoto licha ya kwamba alikuwa kwenye ndoa. Ushauri nasaha ulimuondolewa hofu hiyo.
“Nimeweza kupata mtoto kupitia kwa msaada wa mwalimu Regina na shirika hili. Nilikaa miaka mingi bila kupata mtoto sababu ya kufikiria sana. Sababu ya kutojisikia kama mimi ni mtu lakini Mungu amesimama na mimi. Kupitia Forum for Women au FODDAJ nikaweza kupata mtoto baada ya kuwa kwa ndoa miaka mingi. Nasema asante kwa Mwalimu Regina.”
Baada ya kupata zawadi hiyo ya mtoto, Geraldine ana ombi kwa Umoja wa Mataifa. Akisema Refugee anamaanisha mkimbizi, na alien card ni kibali cha ukazi.
“Naomba Umoja wa Mataifa uweze kusimama na sisi kama wakimbizi, waweze kutusaidia. Mara nyingi mimi siwezi kupata mengi ya kufanya bila kupitia mwananchi hapa Kenya. Lazima nipitie Mkenya ili nipate kibali na nipate jinsi ya kuweza weka duka hata kama ni kibanda, lazima nipitie Mkenya nimuombe anishike mkono twende anifikishe pale ili niweze kujitetea pale mbele. Lakini mkisimama na sisi tutaweza kujitetea kwa upande wa serikali, tutaweza kupata matibabu. Watoto wakiwa wagonjwa tunaweza kwenda hospitalini waweze kusaidiwa kwa matibabu kirahisi.