
Kila nchi katika Umoja wa Ulaya (EU) inatakiwa kutambua ndoa za watu wa jinsia moja moja iliyofungwa katika nchi nyingine mwanachama, kulingana na uamuzi wa Mahakama ya Haki ya EU (CJEU) uliotolewa leo Jumanne, Novemba 25.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mahakama hiyo ilipokea malalamiko kutoka kwa raia wawili wa Poland waliofunga ndoa nchini Ujerumani ambao walikataliwa kusajiliwa kwa cheti chao cha ndoa katika nchi yao ya asili, ambapo ndoa ya jinsia moja hairuhusiwi, shirika la habari la AFP limeripoti.
Nchi zote za Umoja wa Ulaya zinahitajika kutambua ndoa za watu jinsia moja zilizofungwa kisheria katika nchi nyingine mwanachama, kulingana na uamuzi wa Mahakama ya Haki ya EU (CJEU) uliotolewaJumanne.
“Haki ya kuheshimiwa kwa maisha ya kibinafsi na ya kifamilia”
Kukataa huku “ni kinyume na sheria ya EU” kwa sababu ni kikwazo kwa uhuru wa raia husika kutembea kutoka nchi moja kwenda nyingine huku wakifurahia haki zao walizopata ndani ya Umoja huo.
“Inakiuka uhuru huu pamoja na haki ya kuheshimiwa kwa maisha ya kibinafsi na ya kifamilia,” CJEU imesema. “Kwa hivyo nchi wanachama zinalazimika kutambua, kwa madhumuni ya kutekeleza haki zilizotolewa na sheria ya EU, hali ya ndoa iliyopatikana kisheria katika nchi nyingine mwanachama,” imeongeza.
Uamuazi huo unafafanua kwamba, hata hivyo, Poland haihitajiki kuingiza ndoa ya jinsia moja katika sheria yake.