Ripoti hiyo iliyochapishwa kwenye Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake inabainisha kuwa  Kila 10 dakika, mwanamke au msichana anauwawa na mpenzi au jamaa.

Mnamo mwaka 2024 imesema wanawake na wasichana 50,000 waliuawa na wapenzi wao wa karibu au wanajamii sawa na mwanamke mmoja kila dakika 10.  Na kuongeza kkuwa Licha ya ahadi za muda mrefu za kimataifa, viashiria havijaboreshwa kwa miaka mingi.

Kulingana na Ripoti ya mauaji ya kijia au Femicides ya 2025, jumla ya wanawake na wasichana 83,000 waliuawa kwa makusudi mwaka jana.

Kati ya hao, asilimia 60 yaani wanawake na wasichana 50,000 waliuawa na wapenzi wao au jamaa.

Hi ini sawa na wastani wa wanawake na wasichana 137 kuuwawa kila siku imesema ripoti hiyo kwa kulinganisha, ni asilimia 11 tu ya wanaume waliouawa na wapenzi wao au jamaa.

Ukatili wa mtandaoni dhidi ya wanawake unaongezeka duniani kote.

© Unsplash/Julio Lopez

Ukatili wa mtandaoni dhidi ya wanawake unaongezeka duniani kote.

Ukatili mtandaoni ni vitisho halisi

“Mauaji ya wanawake hayaji tu. Mara nyingi huwa matokeo ya ukatili unaoendelea unaoanza na udhibiti, vitisho, na unyanyasaji ikiwa ni pamoja na mtandaoni,” amesema Sarah Hendricks, Mkurugenzi wa Sera, Programu, na Mahusiano ya Serikali na Serikali kwa UN Women.

Amesisitiza kwamba kampeni ya Siku 16 za Uhamasishaji wa Hatua ya mwaka huu inalenga kuonesha jinsi ukatili wa kidijitali mara nyingi unavyopanuka kutoka mtandao hadi vitisho vya kimwili na, katika kesi mbaya zaidi, kupelekea mauaji.

“Kila mwanamke na kila msichana ana haki ya usalama. Kuzuia mauaji ya wanawake kunahitaji hatua za haraka na kutekeleza sheria zinazoshughulikia ukatili mtandaoni na nje ya mtandao,” ameongeza Hendricks.

Nyumbani bado ni mahali hatari kwa wengi

John Brandolino, Kaimu Kiongozi wa UNODC, amebainisha kuwa “Nyumbani bado ni sehemu hatari, na wakati mwingine kwenye kifo, kwa wanawake na wasichana wengi. Ripoti hii inaonesha haja ya hatua madhubuti zaidi za kuzuia mauaji ya wanawake na kuimarisha hatua za mifumo ya haki za jinai.”

Wanawake wanasema hapana kwa unyanyasaji.

© Unsplash/Nadine E

Wanawake wanasema hapana kwa unyanyasaji.

Kulingana na ripoti hiyo, matukio ya mauaji kwa msingi wa jinsia yameandikwa katika kila eneo la dunia.

Kiwango kikubwa cha mauaji ya wanawake yanayofanywa na wapenzi au jamaa kinakadiriwa kuwa barani Afrika ambako kesi 3 kwa kila wanawake na wasichana 100,000. Kanda zingine zinazofuata ni Amerika 1.5, Oceania 1.4, Asia 0.7, na Ulaya 0.5.

Uhaba wa takwimu na uboreshaji wa ufuatiliaji

Ingawa baadhi ya mauaji hutokea nje ya nyumba, takwimu kuhusu matukio haya bado ni hafifu imesema ripoti.

Ili kuboresha ufuatiliaji na uchambuzi, UN Women na UNODC zinafanya kazi na nchi mbalimbali kutekeleza mfumo wa takwimu utakaoruhusu utambulisho sahihi, urejeshaji, na uainishaji wa mauaji yanayozingatia jinsia.

Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba kuboresha wingi na ubora watakwimu ni muhimu kwa kutathmini kiwango cha tatizo, kuunda hatua madhubuti, na kuhakikisha upatikanaji wa haki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *