Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kuwa mashambulio ya makundi ya wanajihadi na ukosefu wa uthabiti kaskazini mwa Nigeria yanasababisha viwango vya baa la njaa kuongezeka.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na WFP, karibia watu Milioni 35 wanatarajiwa kukabiliwa na uhaba wa chakula mwaka ujao wa 2026.
Katika jimbo la Borno, kitovu cha mzozo wa miaka 16 sasa, karibia watu Elfu 15 wanatarajiwa kukabiliwa na baa la njaa au dalili kulingana na WFP.
Mzozo wa kaskazini mwa Nigeria umesababisha vifo vya zaidi ya watu Elfu 40 wakati wengine Milioni 2 kaskazini mashariki mwa nchi wakipoteza makazi yao, mzozo ambao hata hivyo umeingia hadi katika mataifa jirani.

Kando na kuwepo kwa kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria, taifa hilo la Afrika Magharibi pia linakabiliwa na utovu mwengine wa usalama unaosababishwa na makundi mengine ya wapiganaji katikati mwa nchi na hata Kaskazini Magharibi.
Makundi hayo yenye silaha yamekuwa yakitekeleza mashambulio katika vijiji tofauti kwenye maeneo hayo wakitekeleza mauaji ya raia na hata kuwateka wengine yakiwa na nia ya kulipwa fidia.
Wiki iliopita, Nigeria yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika iliripoti matukio matatu ya utekaji wa watu.

Zaidi ya wanafunzi 300 na Walimu wao walitekwa kutoka katika shule inayomilikwa na kanisa Katoliki katika jimbo la Niger.
Katika tukio lengine, wanafunzi 25 wa kike walitekwa kutoka katika shule nyengine jirani katika jimbo la Kebbi.
Wahuni 38 walitekwa wakati wakiendelea na ibaada yao iliyokuwa ikiperushwa moja kwa moja katika jimbo la Kwara.