
Upungufu mkubwa wa ghafla wa misaada ya kimataifa ya VVU mwaka 2025 umeongeza mapungufu ya ufadhili yaliyokuwepo tayari. Shirika la Muungano wa Ulaya la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) inakadiria kuwa msaada wa afya kutoka nje unatarajiwa kupungua kwa 30–40% mwaka 2025 ikilinganishwa na 2023, jambo linalosababisha kuvurugika mara moja na kwa kiwango kikubwa zaidi kwa huduma za afya katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati.
Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS anasema, “janga la ufadhili umeonesha udhaifu wa maendeleo ambayo tumepigania kwa bidii kuyafanikisha . Kila nukta ya data katika ripoti hii inawakilisha watu, watoto wachanga waliokosa uchunguzi wa VVU au utambuzi wa mapema wa VVU, wanawake vijana waliokataliwa msaada wa kuzuia, na jamii ambazo ghafla zimebaki bila huduma na matunzo. Hatuwezi kuwaachia. Lazima tutokomeze janga hili na kubadilisha majibu ya UKIMWI.”
Mfumo wa ulimwengu ukiwa katika mshtuko
Huduma za kuzuia VVU ambazo tayari zilikuwa na changamoto kabla ya janga ndizo zilizoathiriwa zaidi. Upungufu mkubwa wa dawa za kuzuia VVU (PrEP) na kupungua kwa upandikizaji wa uzazi wa kiume kwa hiari kumeacha pengo kubwa la ulinzi kwa mamilioni. Kufutwa kwa programu za kuzuia VVU zilizoundwa kwa kushirikiana na vijana wa kike na wanawake kumewapunguzia wasichana na wanawake vijana upatikanaji wa huduma za kuzuia VVU, afya ya akili, na kuzuia unyanyasaji wa kijinsia katika nchi nyingi. Hali hii inaongeza hatari yao zaidi. Tayari mwaka 2024 kulikuwa na maambukizi mapya ya HIV 570 kila siku miongoni mwa wasichana na wanawake vijana wenye umri wa 15–24 duniani.
Mashirika yanayoendeshwa na jamii ambayo ndizo nguzo ya majibu ya VVU na zilikuwa na uwezo wa kufikia watu walio hatarini zaidi yameripoti kufungwa kwa jumla, na zaidi ya 60% ya mashirika yanayoongozwa na wanawake yamekoma kutoa programu muhimu. Huduma kwa makundi muhimu ikiwemo wanaume wanaoshirikiana kimwili na wanaume wnzao, wafanyabiashara wa ngono, watu wanaotumia sindano za dawa za kulevya, na watu wa jinsia tofauti pia zimeathirika vibaya.
Kushindwa kufikia malengo ya kimataifa ya VVU ya 2030 ya Mkakati unaofuata wa Global AIDS kunaweza kusababisha maambukizi mapya milioni 3.3 kati ya mwaka 2025 na 2030.
Masuala yanayohusiana na haki za binadamu
Mgogoro wa fedha umetokea sambamba na hali mbaya ya haki za binadamu duniani, haswa kwa makundi yaliyo hatarini. Mwaka 2025, idadi ya nchi zinazoruhusu uhalifu kwa shughuli za ngono za jinsia moja na maonesho ya kijinsia imeongezeka kwa mara ya kwanza tangu UNAIDS ilipoanza kufuatilia sheria za adhabu mwaka 2008. Vizuizi kwa mashirika ya kiraia, haswa yale yanayofanya kazi na makundi muhimu na wanawake na wasichana vijana barani Afrika, vinaathiri upatikanaji wa huduma muhimu za VVU.
Ujasiri na ubunifu hutoa tumaini
Licha ya changamoto hizi, baadhi ya nchi zimechukua hatua za haraka kufunika pengo la fedha. Hii imewezesha nchi nyingi kuonesha uthabiti katika utoaji wa tiba za VVU. Baadhi ya nchi zimeripoti idadi thabiti au hata ongezeko la wagonjwa wapya wanaoanza tiba ya antiretroviral (ART).
Nigeria, Uganda, Côte d’Ivoire, Afrika Kusini, na Tanzania zote zimeahidi kuongeza uwekezaji wa ndani katika huduma za VVU. UNAIDS inashirikiana na nchi zaidi ya 30 kuharakisha mipango ya kudumu ya kitaifa.
Ubunifu pia unaongezeka. Teknolojia za kuzuia VVU ikiwa ni pamoja na sindano mbili kwa mwaka za kuzuia maambukizi zinaweza kuzuia maambukizi mapya kwa mamilioni katika maeneo yenye mzigo mkubwa. Ushirikiano mpya wa mwaka 2025 ulioanzishwa na Gates Foundation, UNITAID, Global Fund, na US PEPFAR unalenga kuhakikisha upatikanaji wa dawa za gharama nafuu, kwa kiasi cha USD 40 kwa mtu kwa mwaka katika baadhi ya kesi.
“Tunajua kinachofanya kazi tuna sayansi, zana, na mikakati iliyothibitishwa. Kinachohitajika sasa ni ujasiri wa kisiasa. Kuwekeza katika jamii, kuzuia, ubunifu, na kulinda haki za binadamu ndiyo njia ya kumaliza AIDS.” Winnie Byanyima, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, amesema.
Mwisho mwa 2025, matukio kama mkakati mpya wa afya ulimwenguni , Marekani na makubaliano na nchi 70, pamoja na ahadi za USD 11.34 bilioni kutoka Mkutano wa 18 wa Global Fund, yanatoa tumaini la kudumisha ufadhili muhimu wa kimataifa wa VVU.
Wito wa Kuchukua Hatua
Leo, watu 40.8 milioni wanaishi na VVU duniani, maambukizi mapya 1.3 milioni yalitokea mwaka 2024, na watu 9.2 milioni bado hawapati tiba.
Siku ya UKIMWI, UNAIDS inawaomba viongozi wa dunia:
- Kudumisha mshikamano wa kimataifa na kujitolea pamoja kumaliza ugonjwa wa UKIMWI
- Kuhakikisha ufadhili wa kimataifa unaendelea ili kusaidia mpito salama kuelekea ufadhili wa kitaifa
- Kuwekeza katika ubunifu na upatikanaji wa dawa nafuu za muda mrefu
- Kulinda haki za binadamu na kuimarisha mashirika yanayoongozwa na jamii
“Huu ni wakati wetu wa kuchagua. Tunaweza kuruhusu mshtuko huu uharibu mafanikio ya miongo, au tukaungana nyuma ya maono ya pamoja ya kumaliza ugonjwa wa UKIMWI. Maisha ya mamilioni yanategemea maamuzi tunayoyafanya leo.” Winnie Byanyima anaonya.