
Mshauri wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu masuala ya Afrika amesema pande hasimu nchini Sudan hazijakubali mapendekezo mpya ya usitishaji wa vita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na Massad Boulos, pande hizo zinatakiwa kukubali mapendekezo hayo ya Washington yaliowasilishwa na wapatanishi wa mzozo huo bila ya marsharti.
Boulos amezungumza katika kikao cha pamoja na wanahabari akiwa na mshauri wa Rais wa UAC He spoke Anwar Gargash jijini Abu Dhabi.
Taarifa ya Bulos imejiri zikiwa zimepita siku chache tangu kiongozi wa serikali ya kijeshi nchini Sudan Abdel Fattah al-Burhan kutupilia mbali mapendekezo hayo yaliowasilishwa naye, Burhan akimtuhumu Boulos kwa kuegemea upande wa UAE.
Burhan alikuwa amekashifu mapendekezo mapya ya kusitisha mapigano kwa msingi kuwa yanaegemea upande mmoja kwenye mzozo wa Sudan.
Sudan imekuwa ikiikashifu UAE kwa kuwahami wapiganaji wa RSF ambao imekuwa ikipigana nao katika mzozo wa uongozi.
UAE imekanusha madai ya Sudan.