Ofisi ya haki ya Umoja wa Mataifa, imesema imeorodhesha visa 2,767 vya ukiukaji wa haki za binadamu na sheria za kimataifa za msaada nchini Kenya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, katika miezi sita ya kwanza mwaka huu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake iliyochapishwa jana, ofisi hiyo ya haki imesema idade hiyo ni ongezeko la asilimia 11 ikilinganisha na miezi sita ya mwisho mwaka jana.

Asilimia 86 ya visa hivyo viliripotiwa katika mikoa inayoendelea kushuhudia machafuko,idade ya waathiriwa ikipanda pia kwa asilimia 12.

Makundi ya waasi ya ADF, CODECO na M23 yamehusishwa na makosa haya, katika maeneo ya Kivu Kusini na Kaskazini pamoja na Ituri.

Katika eneo la Ituri, visa 416 viliripotiwa, hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 21 ikilinganishwa na mwaka jana,ADF ikitajwa kuchangia visa 198.

Aidha vikosi vya serikali vinatuhumiwa kwa udhalilishaji wa kingono, dhidi ya waathiriwa 69.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *