
Mafuriko na maporomoko ya ardhi nchini Sri Lanka, yaliyosababishwa na mvua kubwa, yamegharimu maisha ya watu wasiopungua 123 na makumi ya maelfu wakilazimika kuhama makazi yao, Kituo cha Usimamizi wa Maafa kimetangaza katika ripoti mpya leo Jumamosi, Novemba 29.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Katika taarifa, Kituo cha Usimamizi wa Maafa cha Sri Lanka (DMC) kimeripoti vifo 123 na watu 130 amba hawajapatikana. Mkurugenzi mkuu shirika hilo, , Sampath Kotuwegoda, amesema kuwa shughuli za uokoaji zinaendelea, akibainsha kwamba karibu watu 44,000 wamehamishwa.
Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na hali mbaya ya hewa tangu siku ya Jumatatu kutokana na Kimbunga Ditwah, ambacho kwa sasa kinaelekea nchi jirani ya India, kulingana na DMC. Mafuriko yamezidi kuwa mabaya leo Jumamosi katika maeneo ya mabondeni, na kusababisha mamlaka kuagiza uhamishaji wa kingo za Mto Kelani, ambao ulivunja kingo zake siku ya Ijumaa jioni.
Mvua imepungua kote nchini, lakini mvua zinaendelea kunyesha kaskazini. Serikali ya Sri Lanka imetuma jeshi kusaidia shughuli za uokoaji.
Maafisa wa DMC wamesema wanatarajia viwango vya mafuriko kuwa juu kuliko vile vilivyorekodiwa mwaka wa 2016, wakati mafuriko yaliwaua watu 71 kote kisiwani humo.