“Azimio la Baraza la Usalama liko wazi  kuhusu kutoita kitu chochote mpaka au vinginevyo, ni kuhusu eneo ambalo linapaswa kuheshimiwa kwa ukamilifu wake,” amesema, akirejelea azimio lililopitishwa Novemba 17 kuunga mkono mpango kamili wa kumaliza mgogoro.

Türk ameziomba pande zote kuheshimu muafaka wa kunyamazisha silaha na kuhakikisha kwamba hatua inayofuata ya mpango wa amani Gaza inaweza kuendelea.

Amesema“Gaza bado ni mahali pa mateso yasiyoelezeka, kupoteza matumaini na hofu. Hata kama damu imepungua kumwagila lakini, haijakoma.”

Mashambulizi yanaendelea na athari zake

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Palestina UNRWA, sehemu kubwa ya vurugu wiki iliyopita imejitokeza karibu na “Mstari wa Njano,” ambapo matofali makubwa ya zege yamehamia, yakiunda “wimbi jipya la wakimbizi”.

Takwimu za mamlaka za afya za Gaza zinaonesha kuwa Wapalestina 360 wameuawa na 922 kujeruhiwa tangu makubaliano ya kusitisha mapigano na kunayamzisha silaha kuanza mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Zaidi ya miili 617 imetolewa chini ya vifusi vya mabaki ya maporomoko ya majengo.

Türk amesema ofisi yake imeorodhesha mashambulizi zaidi ya 350 tangu mapumziko ya silaha kuanza, wakiwemo wanawake saba na watoto 13. “Mashambulizi ya Israel yanaendelea, ikiwa ni pamoja na watu wanaokaribia Mstari wa Njano, kwenye majengo ya makazi, makazi ya wakimbizi wa ndani [IDP] na kwenye miundombinu mingine ya kiraia,” Tuk ameviambia vyombo vya habari.

Janga la afya ya akili

Mkuu huyo wa Haki za Binadamu amesisitiza kwamba janga la kisaikolojia linaloathiri wakazi wa eneo hilo ni “mgogoro mkubwa wa afya ya akili uioweza kufikiriwa. Kimsingi kila mtu amekumbwa na mshtuko, hasa watoto.”

Katika mkutano wa waandishi wa habari ulioadhimisha Siku ya Haki za Binadamu, hii leo Türk pia ameonesha wasiwasi mkubwa kuhusu “viwango vya kushambuliwa bila kifani na vikosi vya Israel na wapangaji wa ardhini dhidi ya Wapalestina” na ardhi yao katika Ukingo wa Magharibi uliozingirwa.

Amesisitiza“Huu ni wakati wa kuongeza shinikizo na utetezi si wakati wa kulegea”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *