Katika mkutano uliofurika waandishi wa habari mjini Geneva, Mkuu huyo wa Haki za Binadamu alichora taswira nzito ya dunia ambako ulinzi wa haki unapungua kwa kasi ya kutisha.

Amesema mfumo wa kimataifa wa haki za binadamu unakosa ufadhili, akionya kuwa Ofisi yake imepoteza takribani dola milioni 90 mwaka huu, hali iliyosababisha kupunguzwa kwa kazi muhimu wakati mahitaji yakiongezeka. Amesema

“Haki za binadamu hazina ufadhili wa kutosha, zinadhoofishwa, na zinashambuliwa  lakini bado zina nguvu, hazijakatishwa tamaa, na zinajipanga upya.”

Türk amekemea kile alichokiita ongezeko la harakati za kupinga haki na kupinga usawa wa kijinsia, wakati faida za kampuni za silaha zikiongezeka kwani kampuni kubwa za silaha duniani zilipata kwa pamoja zaidi ya dola bilioni 679 mwaka jana.

Ameonya pia kuhusu kuzorota kwa hali ya migogoro kuanzia Gaza hadi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Sudan na Ukraine ambapo raia wanaendelea kubeba mzigo wa machafuko hayo. Ameongeza

SOT 2 – Türk: “Upinzani dhidi ya haki za binadamu nao unakabiliwa na upinzani unaongozwa na vijana wanaokataa ufisadi, ukandamizaji na ukosefu wa usawa.”

Türk amesema hakuna amani endelevu inayoweza kupatikana bila haki za binadamu kuwa kiini cha jitihada, akizisihi serikali zisikandamize maandamano bali yazitazame kama fursa za mageuzi. Amesisitiza

SOT 3 – Türk: “Huu ni wakati wa kuongeza shinikizo kwa ajili ya haki si wakati wa kulegea.”

Licha ya hali ngumu, amesema anatiwa moyo na harakati za kijamii duniani kote, na ameahidi kuwa mapambano ya utu na usawa yataendelea.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameadhimisha Siku hii ya Haki za Binadamu kwa kutoa wito wa umoja wa kimataifa katika kulinda haki za msingi.

Amesema Tamko la Ulimwengu la Haki za Binadamu, lililopitishwa takribani miaka themanini iliyopita, bado ni msingi wa dunia inayolenga kuhakikisha kila mtu anaishi na kustawi.

Lakini ameonya kuwa nafasi za kiraia zinazidi kupungua na ukiukaji mkubwa unaonesha kutoheshimiwa kwa haki na kutojali mateso ya binadamu.”

Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa  amesema shirika la Umoja wa Mataifa likishirikiana na serikali na asasi za kiraia, hutoa chakula, makazi, elimu, amani na ulinzi kila siku lakini haliwezi kufanya kazi hiyo pekee. Amewataka watu kila mahali kusimama na kutetea walio hatarini zaidi, akisisitiza kuwa haki haziwezi kamwe kuwa ya pili baada ya faida au nguvu.

Na jijini Nairobi Kenya siku hii imeadhimishwa kwa mafunzo maalum kwa vijana kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu mtandaoni na athari zeke huyu ni mmoja wa walioshiriki

Kauli mbiu ya Siku yam waka huu ni “Haki ni msingi wa kila siku” 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *