Wizara ya Afya na Huduma za Kibinadamu ya Marekani imetangaza kwamba Idara ya Chakula na Dawa (FDA) inafanya uchunguzi wa kina kuhusu vifo vinavyoweza kuhusishwa na chanjo za COVID-19, vinavyohusisha makundi mengi ya umri.

Msemaji wa wizara hiyo, Andrew Nixon, amesema kwamba makundi ya umri yanayochunguzwa bado hayajawekwa wazi.

Hapo awali Kamishna wa FDA, Marty Makary alisema kwamba shirika hilo lilikuwa likichunguza vifo hivyo miongoni mwa tabaka la vijana.

Afisa mkuu wa matibabu na masuala ya kisayansi wa Idara ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA), Vinay Prasad, alieleza katika taarifa ya mwezi uliopita kwamba kuna uwezekano chanjo hizo zilichangia vifo vya watoto wasiopungua 10 kutokana na ugonjwa wa myocarditis, kwa mujibu wa uchambuzi wa awali wa vifo 96 kati ya 2021 na 2024.

Matokeo haya hayakuchapishwa katika jarida la kisayansi lenye hadhi, wala hayakujumuisha maelezo kuhusu hali za kiafya za waathiriwa au makampuni yanayotengeneza chanjo hizo.

Tangazo hilo liliambatana na ripoti zilizochapishwa na Bloomberg na Washington Post uhusu vifo vinavyoweza kuhusishwa na chanjo za COVID-19.

Mwishoni mwa mwezi Novemba, The New York Times iliripoti kwamba Idara ya Chakula na Dawa ya Marekani ilisema katika taarifa ya ndani kwamba kwa uchache watoto 10 huenda wamefariki dunia “kwa sababu ya” chanjo za COVID-19, ikitaja myocarditis kama chanzo kinachodhaniwa cha matukio hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *