
Marekani imewawekea vikwazo watu wanne wa Colombia na makampuni manne kwa jukumu lao la kuajiri mamluki kwa kuelekea Sudan. Wizara ya Fedha ya Marekani ilitangaza hili siku ya Jumanne, Desemba 9. Mapema mwezi Septemba, mamlaka katika Port Sudan ilimwandikia Mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukemea mtandao huu wa Colombia, ambao, kulingana na jeshi la Sudan, unafadhiliwa na Falme za Kiarabu kwa manufaa ya Vikosi vya Msaada wa Haraka.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu jijini Nairobi, Gaëlle Laleix
Kulingana na Wizara ya Fedha ya Marekani, mtandao huu wa mamluki unahusishwa Alvaro Andres Quijano Becerra, mwanajeshi wa zamani wa Colombia na mwanzilishi wa kampuni ya A4SI, ambayo inawaajiri wanajeshi wa zamani wa Colombia kwa ajili ya misheni nchini Sudan. Alvaro Andres Quijano Becerra anaishi katika Falme za Kiarabu.
Kulingana naWizara ya Fedha ya Marekani, aliwahi kuhusika na genge la wahalifu la Norte del Valle. Watu wengine waliowekewa vikwazo ni wale walio karbu naye, ikiwa ni pamoja na mkewe, mkurugenzi wa kampuni ya kuajiri, na raia mwingine wa Colombia ambaye amekuwa akisimamia mishahara ya mamluki.
Marekani inalenga “mtandao unaoajiri mamluki kwa faida ya Vikosi vya Msaada wa Haraka,” anaelezea John Hurley, Naibu Waziri wa Fedha, ambaye analaani “ukatili” wao.
Kwenye ukurasa wake wa Twitter, Cameron Hudson, mtafiti katika Kituo cha Mafunzo ya Kimataifa na Mikakati, anaita vikwazo hivi “kuwa vya kijinga,” ikizingatiwa kwamba utawala wa Trump “hautaji kamwe utawala unaosaini mikataba na kulipa bili.”
Kwa miezi kadhaa, jeshi la Sudan limeishutumu Falme za Kiarabu kwa kufadhili mamluki wa kigeni nchini Sudan. Mjumbe maalum wa Marekani kwa Afrika, Massad Boulos, alikuwa Abu Dhabi mwishoni mwa mwezi Novemba.