
Watu 22 wafariki, 16 wajeruhiwa baada ya majengo mawili kuporomoka katika mji wa Fes, Morocco
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i134170-watu_22_wafariki_16_wajeruhiwa_baada_ya_majengo_mawili_kuporomoka_katika_mji_wa_fes_morocco
Watu wapatao 22 wamefariki dunia na wengine 16 wamejeruhiwa wakati majengo mawili ya makazi ya watu kuporomo katika mji wa Fes ulioko kaskazini mwa Morocco, jana Jumatano.
2025-12-11T06:11:21+00:00 (last modified 2025-12-11T06:11:21+00:00 )
Dec 11, 2025 06:11 UTC
Watu wapatao 22 wamefariki dunia na wengine 16 wamejeruhiwa wakati majengo mawili ya makazi ya watu kuporomo katika mji wa Fes ulioko kaskazini mwa Morocco, jana Jumatano.
Kwa mujibu wa chombo cha habari cha eneo hilo, majengo hayo ya ghorofa mbili kila moja, yaliporomoka katika eneo la Al-Massira ambacho ni kitongoji kilichoko katika mji huo.
Chombo cha habari cha serikali ya Morocco 2M kimesema, vikosi vya uokoaji vilikuwa eneo la tukio vikiendelea kutafuta manusura wa tukio hilo.
Hadi sasa, hakuna taarifa zozote kuhusu chanzo cha ajali hizo.
Majeruhi wa tukio hilo waliwahishwa mahospitalini, huku wakazi wa maeneo jirani wakihamishwa kutoka kwenye nyumba zao.
Waendesha mashitaka nchini Morocco, wametoa amri ya kuanza mara moja uchunguzi wa kubaini chanzo cha mkasa huo…/