Wizara ya ya Iran Usalama na Intelijensia ya Iran imewatia mbaroni watu saba wanaohusishwa na makundi yenye uadui na Jamhuri ya Kiislamu ambayo yana makao yao Marekani na barani Ulaya.

Shirika la habari la Idara ya Mahakama la Mizan lilitoa ripoti hiyo jana Jumatano, likinukuu chanzo chenye taarifa ya suala hilo kutoka ndani ya wizara hiyo.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, watano kati ya watu hao waliotambuliwa na kukamatwa walikuwa wakiwasiliana na kinara wa waungaji mkono wa utawala wa kifalme uliopinduliwa wanaoipinga Iran ambao wana makao yao nchini Marekani.

Wafuasi hao wa utawala wa zamani wa kifalme nchini Iran wamekuwa kwa miongo kadhaa wakiendesha bila mafanikio kampeni ya kujaribu kuurejesha madarakani utawala wa zamani wa kidikteta wa Pahlavi uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani.

Utawala huo uliondolewa madarakani kupitia maandamano makubwa ya umma yaliyofanyika nchini kote mwaka 1979 chini ya uongozi wa mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu hayati Ayatullah Ruhullah Khomeini, ambaye aliongoza wananchi wa Iran katika harakati za kufanikiisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya kihistoria kuwahi kutokea katika nchi hiyo.

Waungaji mkono hao wa utawala wa kifalme, ambao wamekuwa wakipatiwa misaada mikubwa na Magharibi na utawala wa kizayuni wa Israel tangu ushindi wa Mapinduzi, walionekana wakishughulika mno pia wakati wa vita haramu na visivyo na sababu vilivyoanzishwa na Israel na Marekani dhidi ya Iran mnamo mwezi Juni.

Chanzo kilichonukuliwa na shirika la habari la Mizan kimetoa taarifa ya kukamatwa watu wengine wawili pia waliohusishwa na makundi ya wapinga Mapinduzi ya Kiislamu yanayoendesha harakati zao barani Ulaya.

Chanzo hicho kimeripoti pia kukamatwa bunduki 100 zilizoingizwa nchini, na kuongeza kuwa silaha hizo zilikuwa zimeletwa kwa sura ya kuonekana kama bidhaa zilizobebwa na wachukuzi wa mpakani. Ripoti hiyo imeeleza kwamba watu waliohusika katika kuwezesha operesheni hiyo ya kuingiza kimagendo silaha hhizo nao pia wametambuliwa na kukamatwa…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *