
Shamdasani amesema “ Tusijifanye kuwa hii ni hatua iliyochukuliwa kutetea haki za binadamu za mtu yeyote……, tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuja pamoja kwa sauti moja na kuweka wazi kwamba hatua hii ilikuwa ni kinyume cha sheria ya kimataifa ambayo iliwekwa na Nchi Wanachama”.
Tukisalia na Venezuela, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya Kiutu OCHA imeeleza inaendelea kuwasaidia wenye uhitaji nchini humo na mwaka jana ili ainisha zaidi ya wahitaji milioni 8.
Msemaji wa OCHA Jens Laerke amewaambia waandishi wa habari jijini Geneva kuwa “
Kati ya hao watu milioni nane, “900,000 wamewekwa katika makundi ya juu sana ya wenye uhitaji wa sekta mbalimbali … kama vile chakula, lishe, elimu, na huduma za afya, kimsingi mambo yote ambayo nchi ya Venezuela halijaweza kutoa kwa raia wake kwa miaka mingi”.
Inaendelea..