
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Wizara ya madini imefuta kwa muda, marufuku iliyokuwa inatekelezwa baada ya kusitishwa kwa shughuli za usafishaji wa madini ya Shaba na Cobalt huko Kolwezi.Kabla ya hatua hii kuanzia siku ya Jumatatu, mji wa Kolwezi ulishuhudia maandamano na machafuko ya wachimba migodi wadogo wadogo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jumatano hii asubuhi, hali ya mvutano bado imeripotiwa mjini Kolwezi , kusini mwa DRC. Tangu Jumatatu hii, wachimbaji wa madini wanadai kuwa wamepungukiwa wateja wao.
Leonard Zama, ni rais wa shirika la haki za binadamu IPDHOR.
“Katika vitongoji vya Kasulo, Tshamanzaka, Cinq ans, Hewa bora na Luilu, wachimbaji wa madini wameleta machafuko. Walipora mali za watu, walifunga barabara na kujeuri raia” alisema Leonard Zama.
Kwa upande wake, rais wa ushirika wa madini , Jean Claude Tshiwewe alilaani kuingilia kati kwa wachochezi . Hata hivyo, kiongozi huyu anapongeza hatua mpya ya Waziri wa Madini.
“Baada ya kuondolewa kwa hatua hii, mambo yanaanza kurejea vizuri . Tunapaswa kutolewa angalau saa 72 ili kuona ni jinsi gani mambo yataendelea. Lakini najua yatakuwa mazuri. Mara hii tutakuwa na mikataba ya moja kwa moja na viwanda vidogo vya usafishaji wa madini.” Alisema Jean Claude Tshiwewe.
Hadi sasa, wachimbaji madini walipitia kwa wasaidizi kutoka kwa China, India, Lebanon kuuza madini. Hatua hii mupya inahusu tu mkoa wa Lualaba. Haut Katanga inapaswa kusubiri matokeo ya kamati ya uchunguzi kama inavyosema wizara ya madini.