Jacque Manoku, Chifu wa Utawala katika kata ya Matembo iliyoko eneo la Beni-Mavivi, jimboni Kivu Kaskazini ameeleza ushirikiano wao na TANZBATT12 na kikosi cha 5 cha Msaada wa Haraka kutoka Tanzania, (TanzQRF) vinavyohudumu chini ya mwamvuli wa Brigedi ya Kujibu Mashambulizi (FIB) ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO.

Chifu wa Kata ya Matembo (Aliyevalia suti katikati) Jacque Manoku akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa vikosi vya TanzBATT 12.

MONUSCO/Habib Shaban

Chifu wa Kata ya Matembo (Aliyevalia suti katikati) Jacque Manoku akiwa katika picha ya pamoja na Makamanda wa vikosi vya TanzBATT 12.

Chifu Manoku alikuwa akizungumza baada ya kikao cha tarehe 3 Januari 2026 kilichopewa jina la “URAFIKI MEETING” kilichoandaliwa na vikosi hivyo.

Ameendelea kuelezea ushirikiano huo ni wa muda gani?

Tangu mwezi Mei mwaka 2013, vikosi vya Tanzania vimekuwa sehemu ya FIB hapa DRC na tathmini inawekwa bayana na wanawake wakazi wa eneo hili.

Miongoni mwa walioshiriki kikao hicho ni Chifu wa Kimila wa Kijiji cha Vemba-Mavivi mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini.

Ameenda mbali kuelezea mapendekezo yao kwa kikao hiki.

Walinda amani wa Tanzania wa Kikosi cha TanzQRF kilicho ndani ya FIB ya MONUSCO wakiwa kwenye doria huko Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC.

Walinda amani wa Tanzania wa Kikosi cha TanzQRF kilicho ndani ya FIB ya MONUSCO wakiwa kwenye doria huko Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC.

Luteni Kanali Mustafa Mkundi ni Kamanda wa Kikosi cha TANZBATT 12, ambaye pia ni Mkuu wa kituo cha vikosi vinavyotoka Tanzania hapa Beni Mavivi. Yeye anazungumzia siri ya utendaji wa vikosi vya Tanzania vinavyolinda amani hapa DRC.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 zinazochangia idadi kubwa ya walinda amani chini ya Umoja wa Mataifa ambapo kwa sasa inashika nafasi ya 11 miongoni mwa mataifa yanayochangia vikosi tangu ianze ushiriki wake mwaka 1990.

Baadhi ya wanawake walioshiriki mkutano wa "Urafiki Meeting" in huko Kivu Kaskazini nchini DRC.

MONUSCO/Habib Shaban

Baadhi ya wanawake walioshiriki mkutano wa “Urafiki Meeting” in huko Kivu Kaskazini nchini DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *