#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kutokea kwa ajali ya gari aina ya Prado lenye namba za usajili SU 37454, mali ya Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), maeneo ya Kwala, Kibaha mkoani humo na kusababisha vifo vya watu wawili, huku wengine wawili wakijeruhiwa na kuendelea kupatiwa matibabu, miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Chalinze.

Akitoa taarifa kuhusu ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Salim Morcase, amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi uliosababisha dereva kushindwa kulimudu gari hilo wakati akishuka katika eneo la mteremko lenye kona, hali iliyosababisha gari hilo kupinduka.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *