#HABARI: Tanzania imeng’ara katika Jukwaa la Kimataifa la Nishati Jadidifu (IRENA) jijini Abu Dhabi kwa kutangaza mafanikio makubwa ambapo upatikanaji wa nishati safi ya kupikia nchini umeongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2021 hadi asilimia 23.2 mwaka 2025. Mhandisi Anita Ringia kutoka Wizara ya Nishati amebainisha kuwa ukuaji huo wa zaidi ya mara tatu ndani ya miaka minne umetokana na uongozi thabiti wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameweka ajenda hiyo kama kipaumbele cha kitaifa na nguzo muhimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.
Katika jitihada za kuendeleza kasi hiyo, Serikali imepanga kutekeleza miradi mikubwa katika mwaka wa fedha 2025/26, ikiwemo usambazaji wa majiko banifu 200,000 na mitungi ya gesi (LPG) zaidi ya 450,000 kwa bei ya ruzuku, pamoja na mfumo wa kulipia majiko ya umeme kupitia bili za TANESCO. Aidha, Tanzania imepiga hatua kwa kupiga marufuku matumizi ya kuni na mkaa katika taasisi za umma zaidi ya 31,000 zinazohudumia watu wengi, uwekezaji unaokadiriwa kugharimu zaidi ya dola bilioni 1 za Kimarekani huku ukiongezewa nguvu na sekta binafsi na mabenki kama NMB na CRDB kupitia mikopo ya riba nafuu.
Mbali na nishati ya kupikia, Tanzania imetumia jukwaa hilo lenye wanachama 171 kuelezea fursa za uwekezaji katika nishati jadidifu, ikibainisha kuwa mchango wa vyanzo hivyo kwenye gridi ya taifa umefikia asilimia 68. Serikali imewaalika wawekezaji wa kimataifa kushirikiana katika ujenzi wa miundombinu, viwanda vya majiko na vifaa, pamoja na miradi ya umeme wa jua kama ule wa Kishapu (MW 150) na vyanzo vya jotoardhi (Geothermal). Tanzania imesisitiza utayari wake wa kushirikiana na taasisi za kimataifa ili kuziba pengo la ufadhili wa nishati safi barani Afrika, ikiunga mkono lengo la kidunia la kufikia GW 11,000 za nishati jadidifu ifikapo mwaka 2030.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.