#HABARI: Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, ametoa tahadhari kuhusu utegemezi wa teknolojia ya Akili Mnemba (AI) kutoka mataifa ya nje, akionya kuwa hali hiyo inahatarisha uhuru wa kidijitali na usalama wa nchi.
Akizungumza nchini India kwenye Mkutano wa 28 wa Maspika wa Bunge wa Jumuiya ya Madola (CSPOC), Mhe. Zungu alisisitiza kuwa utegemezi mkubwa kwa kampuni za kigeni unaziweka nchi katika hatari ya kupoteza uwezo wa kulinda faragha za wananchi na usalama wa taifa.
Mhe. Zungu alibainisha kuwa taarifa za wananchi zinapomilikiwa na kampuni za nje, nchi inapoteza mamlaka yake na inaweza kutumika kama silaha ya kisiasa kupitia vikwazo vya kiteknolojia. Alieleza kuwa ni muhimu kwa mataifa yanayoendelea kuwa na udhibiti kamili wa mifumo yao ya kiteknolojia badala ya kuwa wapokeaji tu, ili kujilinda dhidi ya shinikizo kutoka kwa mataifa yenye nguvu duniani.
Aidha, alihimiza nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kushirikiana katika kujenga miundombinu yao wenyewe na kutunga sheria za pamoja za kulinda rasilimali za kidijitali. Mhe. Zungu alihitimisha kwa kutoa wito wa kuwepo kwa uwiano sahihi kati ya ubunifu wa teknolojia na usimamizi wake, ili kuhakikisha maendeleo ya AI hayaji kuathiri uhuru na uchumi wa nchi husika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.