
Wizara ya Vita ya Marekani (Pentagon) imewaamuru wanajeshi wapatao 1,500 walio kazini wawe tayari kutumwa kwenda kukandamiza maandamano huko Minnesota.
Maafisa wa wizara hiyo waliliambia gazeti la The Washington Post Jumamosi kwamba, baada ya onyo la Trump, Pentagon imeamua kuwaandaa baadhi ya wanajeshi kwa ajili ya uwezekano wa kupelekwa Minnesota.
Baada ya kuuawa kwa mwanamke asiye na hatia na mawakala wa uhamiaji kuzua maandamano ya hasira huko Minnesota, Rais wa Marekani Donald Trump alisema angeliamilisha ‘Sheria ya (Kupambana na) Uasi’.
Alisema wiki iliyopita kwamba, anajiandaa kutuma wanajeshi kuwasaidia mawakala wa Idara ya Uhamiaji na Forodha (ICE) huko Minnesota “kufanya kazi yao.”
Kupigwa risasi mama wa watoto watatu na wakala wa ICE kumesababisha maandamano makubwa katika miji mikubwa na miji mingine kote Marekani.
Makamu wa Rais wa Marekani, JD Vance na msemaji wa Masuala ya Usalama wa Marekani, Tricia McLaughlin walimpongeza afisa huyo na kudai kupitia mtandao ya kijamii wa X kwamba Ross alifyatua risasi kujilinda.
Katibu wa Habari wa Ikulu ya White House, Karoline Leavitt, amesema Trump ndiye afisa pekee wa Marekani aliyeidhinishwa kuamua iwapo wapeleke wanajeshi huko Minnesota au la, na lini.