#HABARI: Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeungana na Watanzania wote kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya zoezi la kupanda miti.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, Aretas Lyimo, amewaongoza watumishi katika zoezi hilo lililofanyika makao makuu, akisisitiza kuwa kupanda miti ni alama ya kulinda maisha na utu wa Watanzania, sambamba na kuenzi maono ya Rais ya kutunza mazingira.
Serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Kusini, imeadhimisha siku hiyo kwa kupanda miti ya matunda katika Shule ya Sekondari Shangani, iliyopo katika Mkoa wa Mtwara.
Shughuli hiyo imelenga kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais kwa uongozi wake huku ikihamasisha vijana na wanafunzi kushiriki katika utunzaji wa mazingira kama njia ya kuimarisha ustawi wa jamii.
Zoezi hilo limehusisha viongozi mbalimbali na wadau wa maendeleo mkoani humo, ambao wamepongeza juhudi za Rais Samia katika kuimarisha sekta mbalimbali nchini. Mamlaka imetumia fursa hiyo pia kukumbusha jamii juu ya umuhimu wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya ili kulinda nguvu kazi ya Taifa na kuhakikisha vijana wanakuwa na afya njema ya kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania