Imeripotiwa kwamba Mshindi wa Tuzo ya Ballon d’Or 2025, Ousmane Dembélé, hana mipango ya kuondoka Psg na kwenda Saudi Arabia kwa sasa.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa akizivuti klabu za Ligi Kuu ya Saudi Arabia baada ya rais wa PSG, Nasser El Khelaifi, kuonya kuwa kila mchezaji anapaswa kuendana na muundo wa mishahara wa klabu.
Kauli hiyo ilitafsiriwa na baadhi ya watu kama onyo kwa Dembélé, wakati PSG ikikaribia kuanza mazungumzo ya mkataba mpya na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Mshambuliaji wa PSG, Ousmane Dembélé. Picha na Mtandao
Hata hivyo, imeelezwa kuwa Dembélé yuko mtulivu kuhusu hali yake ya baadaye ndani ya PSG.
Ana uhusiano mzuri na rais wa klabu pamoja na kocha Luis Enrique, ameridhika kuwa klabuni hapo na amejikita kikamilifu katika kuwatumikia.
Bado ana miaka miwili na nusu kwenye mkataba wake, na hadi sasa hakuna mazungumzo yaliyoanza kuhusu mkataba mpya wala kiasi chochote cha fedha kilichojadiliwa.
Dembele amekuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha PSG alichojiunga nacho mwaka 2023 akitokea Barcelona kutokana na mchango wake katika kuzalisha mabaon ndani ya timu hiyo.
Mshambuliaji wa PSG, Ousmane Dembélé. Picha na Mtandao
Katika mechi 185 alizoitumikia PSG tangu alipojiunga nayo, nyota huyo wa timu ya Taifa ya Ufaransa ameshahusika na mabao 82, akifunga mabao 40 na kupiga pasi 82 za mwisho.
Msimu huu pekee ameshahusika na mabao nane katika mechi 11 za timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa ambapo amefunga mabao matano na kupiga pasi tatu za mwisho.