#HABARI: Siku moja baada ya Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega, kueleza bungeni mikakati ya serikali ya kuboresha barabara kuu ya Kibaha hadi Chalinze, wakazi na wasafirishaji mkoani Pwani wametoa maoni mseto wakihimiza utekelezaji wa haraka kwa vitendo.
Wakizungumza na ITV Digital, wananchi na wasafirishaji hao wamebainisha kuwa kuchelewa kwa matengenezo hayo kunakwamisha shughuli za kiuchumi na kijamii kutokana na msongamano na ubovu wa miundombinu, huku wakisisitiza kuwa ahadi hiyo ya serikali inapaswa kuanza kutekelezwa mara moja ili kuleta unafuu.
Aidha, watumiaji wa barabara inayoelekea Hospitali ya Tumbi wameiomba serikali kuikarabati barabara hiyo kwa dharura ili kuondoa mashimo yaliyokithiri ambayo yamekuwa chanzo cha ajali za mara kwa mara na uharibifu wa vyombo vya moto.
Katika majibu yake bungeni, Waziri Ulega amesisitiza kuwa serikali imejipanga kikamilifu kutatua changamoto hizo za miundombinu ili kuimarisha usalama wa wasafiri na kuchochea kasi ya maendeleo katika ukanda huo wa Pwani na nchi nzima.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.