Katika kuendelea kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya, Shirika lisilo la kiserikali SOLIDARMED limefanya maboresho ya miundombinu ya wodi ya wazazi na watoto katika Hospitali ya St. Francis, iliyopo Halmashauri ya Mji Ifakara, Mkoani Morogoro, Maboresho ambayo yamegharimu zaidi ya shilingi milioni mia moja, yakilenga kuboresha mazingira ya huduma za uzazi na afya ya mtoto.

Akizindua rasmi wodi hizo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Kighoma Malima, amesema kazi iliyofanywa na SOLIDARMED ni kubwa na ya mfano, huku akilipongeza shirika hilo kwa mchango wake katika kuboresha huduma za afya na kuwajali wananchi.

Kwa upande wake, Meneja wa Mradi wa SOLIDARMED, Maineste James, amesema mradi huo unalenga kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga kwa kuboresha huduma za kujifungua pamoja na utekelezaji wa afua mbalimbali za afya ya uzazi.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya MT. Fransisko Solanus Fussy, amesema maboresho hayo yameleta manufaa makubwa kwa hospitali hiyo, hususan katika kuongeza uwezo wa kutoa huduma bora na salama kwa akina mama na watoto.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *