Uzinduzi wa miaka 49 tangu kuanzishwa kwa chama hicho, Mwenyekiti wa chama cha Mapindizi CCM Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joseph Masunga akiwa katika uzinduzi wa Sherehe hizo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro amesema miaka 49 ya CCM imejaaa mafanikio na amani kubwa kote nchini.

Akizindua sherehe za kumbukizi ya miaka 49 tangu Chama hicho kilipoanzishwa mwaka 1977 Mhandisi Masunga amesema mafanikio hayo hayajatokea kwa bahati mbaya mbali ni uchapakazi, ushirikiano na nidham nzuri ya viongozi wa Chama hicho.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapindizi CCM Mkoa wa Morogoro Nuru Ngereja amesema sherehe za miaka 49 ya CCM zinapaswa kusherehekewa nchi nzima kutokana na uongozi bora wa Nchi hii unatokana na CCM ambao ndio wanaongoza Taifa kwa amani, utulivu na maono makubwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Maulidi Dotto akitoa salam za Mkoa kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima amsema kama Serikali wataendelea kushirikiana na viongozi wote wa Cham hicho ili kuweza kufikia matarajio ya wananchi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *