Serikali kupitia Wizara ya Afya imezindua mashine ya kisasa ya PET Scan katika Hospitali ya Ocean Road, hatua inayotarajiwa kuboresha kwa kiwango kikubwa huduma za uchunguzi na tiba ya ugonjwa wa saratani nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Akizungumza katika hospitali hiyo, Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema mashine hiyo yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 18.7 ina uwezo wa kugundua ugonjwa wa saratani mapema, kubaini hatua ya ugonjwa pamoja na kufuatilia maendeleo ya tiba kwa wagonjwa.
Mhe. Mchengerwa amesema mashine hiyo ni ya kwanza kwa ubora wake katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku akibainisha kuwa nchi chache jirani zina mashine zinazofanana lakini zisizo na teknolojia ya juu kama hiyo iliyofungwa nchini Tanzania.
(Feed generated with FetchRSS)