
Mamilioni ya wafanyakati nchini humo na watoto wanaokwenda shule wanaotegemea usafiri wa Umma, walilazimika kutafuta njia mbadala ya kufika kazini na shuleni katika kipindi hiki cha baridi kali.
Majimbo 15 kati ya 16 yanayounda Ujerumani yataathirika pakubwa na mgomo huo. Jimbo moja tu la Lower Saxony, ndilo lililonusirika kutokana na wafanyakazi wa usafiri wa Umma huko kuamua kutoshiriki mgomo huo.
Verdi inadai mazingira bora ya kazi, ikiwemo muda mfupi wa kazi na wakati mrefu wa mapunziko. Pia inataka nyongeza ya pesa za ziada kwa wafanyakazi wanaofanya kazi usiku na mwishoni mwa Juma.
Kulingana na chama hichomajadiliano pia yanayoendelea kuhusiana na nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi wa majimbo ya Bavaria, Brandenburg, Saarland na Thuringia.